Sunday, 30 September 2012

VURUGU KANISANI: ASKOFU MOKIWA ANUSURIKA KIPIGO KUTOKA KWA WAUMINI, AOKOLEWA NA POLISI

ASKOFU  Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania  la  Dk. Valentino  Mkowa leo amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kunusurika kupata kipigo kutoka kwa waumini wake waliokuwa wenye hasira kali.

Vurugu kubwa ziliibuka mara  baada ya kusomwa kwa  tamko lililothibitisha kuwa nyumba ya maaskofu inamtambua  Askofu Canon Kasagara kuwa ni kiongozi wao halali wa kanisa la Anglikana la watakatifu wote Jimbo  la Ziwa Rukwa mjini Sumbawanga.

Katibu mkuu wa Anglikana Dk, Dickson Chilongani ndiye aliyesoma tamko hilo mara baada ya kumalizika kwa ibada iliyoongozwa na Askofu Mkuu Dk. Mokiwa.

Akisoma tamko hilo Katibu Mkuu alisema kuwa sehemu ya hoja za msingi kamati ya usimamizi wa kanisa hilo zilidai kuwa uchaguzi uliomweka madarakani Askofu Kasagara uligubikwa na rushwa,si za kweli na  nyumba ya maaskofu imeshindwa kuthibitisha hilo hivyo Kasagara ni askofu wao halali.

Kutokana na kauli hiyo waumini hao, walianza kupiga kelele ya kupinga maelezo hayo hali iliyosababisha mjumbe  wa Kamati ya kusimamia kanisa hilo Flugence Lusunzu aliposhika kinasa sauti na kueleza kuwa wanao ushahidi wa kutosha kuwa rushwa ilitumika kwenye kinyang’anyiro cha  uchaguzi huo uliofanyika zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Alidai kuwa uamuzi wa nyumba ya maaskofu haukuwapa fursa ya kusikiliza upande wa walalamikaji ili hali ushahidi upo wazi, kutokana kauli hiyo zilianza fujo zilisababisha askofu Mokiwa kutolewa lugha chafu, kuvuliwa kufia yake ya kiaskofu, huku wengine warusha viti ambavyo alivikwepa hado alipoondolewa akiwa chini ya polisi waliokuwa wamevalia kiraia.

Hali hiyo iliharibu amani iliyokuwa imetawala ndani ya Kanisa hilo ambapo uligeuka kuwa uwanja wa vita huku waumini wakisikika wakidai kuwa ni heri kanisa hilo lifungwe kuliko Askofu Kasagara kuliongoza.

Awali tangu nyakati za asubuhi, polisi waliovaa kiraia walitanda katika viunga vya kanisa hilo ambapo Askofu Mokiwa aliwasili na kulakiwa vizuri na waumini wake waliokuwa wakishangilia kwa nyimbo na mapambio.

Hata hivyo tayari waumini wa Kanisa hilo walionya kwamba askofu Kasagara asikanyage kwenye eneo hilo, kwani kufanya hivyo kunge hatarisha amani onyo ambalo upande wa askofu Kasagara walitii hivyo askofu huyo mwenye makazi yake wilayani Mpanda alibaki katika nyumba moja ya kulala wageni alikokuwa amefikia.

Mmoja wa waumini  Julius Michael alisema kwa kuwa waumini wa Jimbo la Rukwa hawamtaki askofu Kasagara hakuna sababu ya kuwalazimishwa lakini  nyumba ya maaskofu inapaswa kuangalia uwezekano wa kuligawa jimbo hilo.

Tayari Serikali imegawa mkoa wa Rukwa na kuzaa ule wa Katavi sasa hakuna umuhimu wa kuwalazimisha waumini wampokee mtu wasiyemtaka nyumba ya maaskofu waanzishe jimbo katika mkoa huo mpya na aongoze Kasagara.

 Alisema iwapo watatumia nguvu kumuweka Askofu huyo Rukwa haitasaidia kitu kwani hawezi kuwaongoza watu wasiotaka kushirikiana nae.

Mgogoro katika Kanisa hilo umedumu kwa zaidi ya miaka miwili sasa ambapo siku za nyuma waumini hao  walimzuia  Askofu  Mkuu,  Dk  Valentino  Mkowa  kumsimika  Askofu  huyo  na  badala  yake  alisikimkwa  tarehe 16, Juni mwaka jana   Mjini  Mpanda.

Kutokana na kujitokeza kwa mgogoro huo, ilifunguliwa  kesi mahakamani ya Hakimu Mkazi Sumbawanga na waumini wa anglikana, Fulgence Rusunzu na Rojas Bendera  na wenzao 191 yenye  namba 11/2011 wakipinga kuchaguliwa kwa askofu Kasagala kuwa kiongozi wa Dayosisi hiyo.
 Mmoja wa waumini wa kanisa la Anglikana la watakatifu wote la mjini Sumbawanga akiwa na jazba wakati wa vurugu zilizoibuka jana mara baada ya kutolewa uamuzi wa nyumba ya maaskofu wa kuridhia  askofu Mathayo Kasagara kuwa kiongozi wao ambapo vurugu kubwa zilizuka na kusababisha askofu Mkuu wa kanisa hilo Dk Mokiwa kuondolewa akiwa chini ya ulizi wa polisi. picha na Mussa Mwangoka
  Waumini wa Kanisa la Anglikana la watakatifu wote mjini Sumbawanga jana wakipiga kelele kupinga uamuzi wa nyumba ya maaskofu wa kuridhia  askofu Mathayo Kasagara kuwa kiongozi wao ambapo vurugu kubwa zilizuka na kusababisha askofu Mkuu wa kanisa hilo Dk Mokiwa kuondolewa akiwa chini ya ulizi wa polisi. PIcha na Mussa Mwangoka
Askofu Mkuu wa Angikana Tanzania,la Dk. Valentino  Mkowa aliyevuliwa kofia ya kiaskofu akiwa chini ya ulinzi wa polisi waliokuwa wamevalia kiraia wakimtoa nje ya Kanisa la Anglikana la watakatifu wote mjini Sumbawanga baada ya kuzuka kwa vuguru kubwa jana. Picha na Mussa Mwangoka

Tanzanian artist Zigua aki-perform kwenye Fall Fest New York, Sept 2012.

Saturday, 29 September 2012

NEW VIDEOS

MAONYESHO YA SARAKASI YA MAMA AFRIKA YAENDELEA KURINDIMA NEW WORLD CINEMA DAR. UZINDUZI WA TIGO MAMA AFRIKA SARAKASI ILIVYOFANA JIJINI DAR


  Moja ya michezo iliyovutia katika Tigo Mama Africa Circus inayoendelea katika ukumbi wa Mancom ndani ya Centre New World Cinema Mwenge.

Pichani Juu na Chini ni mfululizo wa maonyesho ya sarakasi ya 'Mama Africa Circus'.



 Pichani Juu na Chini ni mfululizo wa maonyesho ya sarakasi ya 'Mama Africa Circus'.
"Karibuni watanzania wote muone sarakasi na utamaduni wa kitanzania".

PRO -24 DJS WAMLETA DNA


PRO -24 Dj’s wameanda tamasha linaloitwa ‘East Afrika pamoja concet’ litakalofanyika tarehe 30 mwezi huu , katika viwanja vya Dar Live tamasha hilo litapambwa na msanii kutoka nchini Kenya 'DNA' anayetamba na kibao kinachojulikana Banjuka na ‘Unamaswali kwani wewe ni Polisi’ Katika tamasha hilo wasanii wa hapa nchini watapata fursa ya kufanya shoo ya pamoja na msanii huyo ili kuongeza radha tofauti ya muziki wa Afrika Mashariki Pro-24 Djs wanaamini kuwa wanakazi kubwa ya kukuza taswira ya muziki wa Tanzania kwani kazi yao ni kutambulisha nyimbo pamoja na kumtambulisha msanii, hivyo hiyo ni njia moja wapo ya kuukuza muziki wetu Kwa njia hiyo ya kuwaleta wasanii tofauti wa nje wanaamini wanakuza muziki kwani msanii huyo anakuja na changamoto ambazo wasanii wa bongo wanajifunza mambo mengi ya muziki PRO- 24 Dj’s ndio kundi la Kwanza la madj nchini Tanzania walioacha kutumia CD katika shughuri zao za muzki na kuendeleza kupiga muziki kwa kutumia vifaa vya kisasa vya Technic Turntable System na Serato vinavyounganishwa na kompyuta 
Kundi hili la Madj ambawo wanapiga muziki wa aina mbalimbali katika kumbi tofauti tofauti za starehe pamoja na kuandaa matamasha huku wakiwaleta wasanii wa nje ya nchi kuja kufanya shoo katika ardhi ya Tanzani Pamoja na hayo kinachowatofautisha Pro-24 Djs na Madj wengine ni kile kitendo cha wao kufanya shoo zao kwa kutumia zaidi mfumo wa kisasa pamoja na kupiga shoo livehuku kukiwa na full shangwe za mashabiki wao kuonyesha kukubali kile kinachofanywa na madj hao Mbali na hayo katika harakati za kukuza muziki wa nchi yetu Pro -24 Djs wanawaleta wasanii wanaofanya vizuri wa Afrika Mashariki, wakiamini kuwa wanaleta changamoto katika tasnia hiyo ya muziki


Sean Paul and Konshens set to rock fans in Uganda

 Sisqo, Demarco and Wayne Wonder held shows in Uganda a few weeks back and now Sean Paul and another Jamaican Garfield Spence aka Konshens are coming to Uganda. Konshens will be performing on October 5, 2012 at Kyadondo Rugby Grounds and Sean Paul will be performing next month at Lugogo Cricket Oval on November 9. Meanwhile, Nigeria’s D’banj and comedian Basket Mouth will also be coming to the country. All these will be competing with the local artistes who equally have album launches 

UPELELEZI HAUJAKAMILIKA KESI YA LULU

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imeambiwa na upande wa Jamhuri kuwa upelelezi wa kesi dhidi ya msanii wa filamu Elizabeth Michael (18) maarufu ‘Lulu’anayekabiliwa na mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba (28) bado haujakamilika Kesi hiyo ilitajwa jana mbele ya Hakimu Augustina Mmbando ambapo upande wa Jamhuri unaendelea kuieleza mahakama hatu za upelelezi wa kesi hiyo, kwamba bado unaendelea Hakimu Mmbando alisema kesi hiyo itatajwa Oktoba 8 mwaka huu na mshtakiwa ataendelea kukaa mahabusu Aidha kwa mujibu wa Mwenendo wa Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA), Lulu hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji lakini mara upelelezi wake utakapokamilika itahamishiwa Mahakama Kuu Tanzania , Kanda ya Dar es Salaa 

ULAYA YASITISHA MSAADA KWA RWANDA


Muungano wa Ulaya umeamua kusitisha msaada kwa Rwanda.
Uamuzi wa Muungano huo umefikiwa kufuatia ripoti ya baraza la usalama la Umoja huo iliyodai kwamba Rwanda inaunga mkono waasi wa M23 dhidi ya serikali ya Congo.
Waasi hao wanadhibiti kimabavu sehemu kubwa ya Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na hata kuwatoza kodi wananchi.
Kundi hilo lilianza uasi katika eneo hilo mwezi Aprili na kusababisha takriban watu nusu milioni kukimbilia usalama wao.
Lakini Rwanda imeendelea kukana madai hayo.
Umoja wa Mataifa unafanya mkutano na baadhi ya yatakayopewa kipaombele kwenye mkutano huo ni swala la mgogoro huo Mashariki mwa Congo.
Mapema mwezi Julai Marekani ilizuia dola 200,000 zilizokusudiwa kulisaidia jeshi la Rwanda.
Msaada wenyewe uliokatwa siyo mkubwa kwa jeshi la Rwanda, lakini hatua hiyo ilitoa ishara kubwa.
Kwa kukata msaada huo, Marekani ni kama ilikuwa inasema "tunaamini ripoti kuwa Rwanda inatibua usalama wa kanda hiyo kwa kuwaunga mkono wapiganaji wa Congo".
Mwezi Juni ,Umoja wa Mataifa ulikabidhi ripoti kwa Baraza la Usalama, ambayo ilisema ina ushahidi mzito kuwa Rwanda inalipatia kundi la M23, wapiganaji na zana, na kurahisisha makamanda wao wakubwa kusafiri na kuvuka mpaka baina ya Congo na Rwanda

NEW VIDEO