Monday, 27 February 2012

50 CENT & BONDIA FLOYD WALIVYOWASILI ORLANDO.


Siku zote Bondia Floyd Mayweather na 50 CENT ambao ni marafiki wakubwa, wamekua wakijionyesha kwa uwezo wa kifedha na mali za kifahari walizonazo, hii picha imetoka wakati wakiwasili Orlando huko Marekani for All-Star weekend, ambapo pia ilikua birthday ya Floyd.
Floyd na 50 ni washkaji sanaaaaa mpaka hata ukiangalia kwenye page yake ya twitter 50 cent anazaidi ya followers Milioni Tano laki tisa lakini yeye anafata page nne tu za twitter, na moja ni ya Floyd Mayweather, lakini pamoja na ushkaji alionao 50 na watu kama Eminem, Dr Dre, na members wake wa G unit kama Lloyd na Tony Yayo hajamfollow hata mtu mmoja kati ya wao…..hapo chini ni List ya page nne tu anazozifata 50 kwenye twitter.

MUGABE ALIVYOSHEREHEKEA BIRTHDAY YAKE!

Matawi ya chama cha ZANU PF cha Rais Mugabe, yalichanga kugharimia sherehe hizo ambazo pia zilikuwa na mashindano ya warembo na mechi ya mpira ambapo rais huyo aliwaambia wafuasi wake kwamba wale wanaopinga msimamo wake dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na ndoa kati yao, wapotelee mbali.
Sherehe za kuadhimisha siku ya kuzaliwa ya Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe kutimiza umri wa miaka 88, zimefanywa katika mji wa Mutare, mashariki mwa nchi hiyo ambapo maelfu ya watu wamehudhuria.
Rais huyo pia alikanusha kuwa ni mgonjwa, ikiwa ni siku kadhaa baada ya kusema atakazana kama kigongo na bado  anaweza kuongoza nchi huku Umri wake pamoja na taarifa kuwa anaugua saratani ya kibofu, zimeshawishi kwamba chama hicho kinahitaji kiongozi mwingine japo chama chake kimemuunga mkono agombee tena urais mwaka huu.

MUONEKANO MPYA WA WILLOW SMITH!

Mtoto wa movie stars Will Smith & Jada, Willow Smith (11) ametoa muonekano wake mpya baada ya kuziwekea rangi nywele zake, mtindo ambao unatumika sana sasa hivi na warembo wengi, ambapo amesema muonekano huo mpya unakwenda sawa na muziki wake mpya na kusisitiza kwamba “nitakua Willow mpya kutoka sasa”

Friday, 24 February 2012

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEB 24











ALIEANDIKA WIMBO MPYA WA CHRIS BROWN & RIHANNA NDIO HUYU, ISOME STORI ALIYOITOA KUHUSU WAWILI HAO


Baada ya single ya Rihanna aliyomshirikisha Chris Brown iitwayo Birthday cake rmx kuanza kupigwa kwenye radio duniani toka ilipotoka wiki hii, Mwandishi/Producer/mwimbaji THE DREAM ambae amehusika kuiandika hiyo track ameamua kuzungumza ukweli.
Amekiri kwa kusema idea ya kumuweka Chris Brown kwenye hiyo track ilitoka kwa Rihanna mwenyewe na anakumbuka yeye, yani The Dream alikua yuko barabarani anaendesha gari huko Miami Marekani alafu Rihanna akampigia simu, akamwambia “nadhani nitamshirikisha Chris kwenye hiyo track, The DREAM  akajibu sijui ni Chris gani unamuongelea, lakini poa sina tatizo na ulichosema…. baada ya hapo Rihanna hakusema kitu na ndio ikaishia hivyo mpaka The DREAM akaja kufaham kwamba ni Chris Brown ndio kapewa mzigo.
Kwa kumalizia The DREAM amesema mbali na kuwa wanafanya kazi pamoja na Rihanna, mwimbaji huyo pia ni rafiki yake wa karibu ndio maana ni rahisi kushirikiana au kuhusisha mawazo kama hayo, ambapo kuhusu mshangao wa wengi kwamba imekuaje Chris Brown na Rihanna wakarudi tena kufanya kolabo wakati kulitokea ugomvi mkubwa kati yao 2009, amesema “tunatakiwa kujifunza kusamehe, na tukisamehe inatakiwa iwe kweli kutoka moyoni sio mdomoni tu”

DMX AWACHANA DRAKE & RICK ROSS.

Rapper DMX amesema kwamba hamkubali kabisa rapper mwenzake yani Drake, ambapo amesisitiza kwamba hampendi Drake wala hamkubali kwa lolote kuanzia stail yake ya kunyoa, mistari yake, hapendi anachoongea, hapendi sura yake wala hapendi anavyotembea.Amesema anapenda kuzungumzia kuhusu kula tu, sasa atakula kiasi gani? Kingine kinachomkera kuhusu Rick Ross ni kujisifia kuwa na magari ya kifahari na kuimba kuhusu utajiri au mali.
Pamoja na kuwachana marapa hao, Dmx amesema hana tatizo na Lil Wyne, uhusiano wao uko poa ambapo hii ishu imetokea wakati akihojiwa na kituo cha power 105 New York Marekani.

KEISHA ARUDI KUFANYA KAZI NA BABTALE WA TIPTOP!


Member wa zamani wa kundi la Tip Top Connection mwimbaji Keisha leo ametangaza kuitoa single yake ya pili kuiandika na kuiimba toka aolewe na kujifungua mtoto ambae ana umri wa zaidi ya mwaka mmoja.
Kingine ambacho kilifanya nishawishike kumuuliza hili swali haraka, ni pale aliposema sasa hivi kwenye hii single anashirikiana kikazi na Meneja wa Tip Top Connection Bab Tale.
Keisha amesema “mambo ya tumbo tuyaweke mbali, sasa hivi tunafanya 

Thursday, 23 February 2012

WACHINA WA MAGUFULI WAHUKUMIWA.


Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam imetoa hukumu ya miaka 10 & 20 kwa raia watano wa CHINA wa kesi maarufu iliyopewa jina la  ‘”SAMAKI WA MAGUFULI’ ambapo pamoja na hukumu hiyo mahakama hiyo imetaifisha Meli waliyokamatwa nayo.
Jaji Augustino Mwajira amesema kwa kuzingatia hoja za wakili wa utetezi na za upande wa utetezi ameamua kuitaifisha meli hiyo kwa manufaa ya umma ili kukomesha uvuvi haramu kwenye ukanda wa Tanzania”
Kuhusiana na washitakiwa katika shitaka la kwanza amewahukumu nahodha wa meli hiyo na wakala wa meli hiyo kulipa faini ya shilingi bilioni moja au kutumikia kifungo cha miaka 20 jela kila mmoja.
katika shitaka la pili mahakama kuu imemtia hatiani nahodha wa meli hiyo kwa kuongoza meli isiyotambulika na kumuhukumu kwenda jela miaka kumi au kulipa faini ya shilingi bilioni 20 ambapo hata hivyo washitakiwa wameruhusiwa kukata rufaa huku Watuhumiwa wengine watatu waliokua wanatetewa na wakili wa kujitegemea wameachiwa huru baada ya mahakama kuwaona kwamba hawana kesi ya kujibu.

ALICHOSEMA DIAMOND KUHUSU ALICHOFANYIWA NA TUZO ZA KILI!!

Wiki mbili baada ya washiriki wa tuzo za KTMA mwaka huu kutangazwa huku Diamond Platnums akiwa amechaguliwa kwenye category nyingi zaidi, msanii huyo amekiri kwamba mpaka sasa ni lazima akubaliwa kwamba Tuzo 3 za KTMA mwaka juzi zimeleta mabadiliko makubwa sana kwenye maisha yake.
Amesema “kwanza zilininyanyua na kujulikana kwenye nchi mbalimbali Afrika na hata nilipokua najitambulisha nilikua najitetea kwa ushahidi wa tuzo hizo”
Naseeb amekubali kwamba kupata tuzo hizo kulimfanya apandishe hata bei ya kupiga showz, “nakumbuka kipindi hiko kwa sababu ndio nilikua naanza nilikua na wimbo mmoja wa kamwambie japokua nilikua nimetoa video ya single ya Mbagala na nilikua nafanya show kwa laki tano mpaka laki sita lakini kwa sasa bei zimebadilika”
Show za Bongo Diamond anaanza kupiga kuanzia milioni 2, na za nje ya nchi ni kuanzia dola    za kimarekani elfu 3mpakaelfu 5.  

POLISI WANNE MBARONI KWA MAUAJI YA RAIA MKOANI RUVUMA

Mtoto Shangwe Mtaula (16) mkazi wa Mabatini akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma alikolazwa baada ya kulipukiwa na bomu la machozi wakati wa vurugu zilizotokea mjini Songea.

call on Jesus every things are possible


Bob Junior a.k.a. Sharobaro - Nanini


HII NDIO PESA ANAYOLIPWA OMMY DIMPOZ KWENYE SHOW!


Hii nafasi nimempa staa wa single ya Nai Nai, Ommy Dimpoz ambae juzi alitangaza kwenye millardayo.com kwamba hawezi kutoa single nyingine mpya kwa sasa kwa sababu nai nai bado inafanya vizuri, huku ikiwa ndio ya kwanza kwenye 20 kali za Clouds Fm.
Stori aliyonayo leo ambayo imenifanya nimpe hii nafasi, ni kitendo chake cha kukubali kutaja pesa anayolipwa kwenye show moja, yani akisimama tu kwenye stage, ujue tayari ameshavuta huo mkwanja.
Ommy amesema sasa hivi ameshapiga showz zisizopungua 15 toka aitoa single ya Nai Nai mwishoni mwa mwaka 2011 na show yake moja kwa Dar es salaam analipwa milioni mbili, kwa mkoani ndio milioni tatu.

MASTAA WA NIGERIA WANAVYOTAMBA NA MAGARI YAO!

                                                Hii ni Bentley mpya ya mkali wa muziki Timaya.
                                                   Chrysler 300 ya mwanamuziki W4.
                                       Hii ndio Porsche Cayenne ya Mchezaji wa timu ya taifa na Rubin Kazan ya Russia Obafemi Martins
  
  Mtandao maarufu wa Nigeria wa Bella Naija, umeandika kwamba kila wiki huwa wanapokea email kutoka kwa mwanamuziki au muigizaji ambae amenunua gari jipya, ni email ambazo huambatana na picha ambapo mastaa wengi bado wanapenda kununua gari aina ya Range Rover.

AY AAMPLIFY KUHUSU KOLABO ZA TYGA WA YOUNG MONEY & YOUNG JOC!


Siku nne baada ya kuthibitisha kupiga kolabo na wakali kutoka Jamaica Tanto Metro na Devonte, Ambewe Yessaya AY amethibitisha kwamba kolabo aliyoipiga mwanzo na Young Joc wa Bad Boy imemalizika, na kilichobaki ni Video tu.
Amesema ” Audio yote iko sawa, yeye ndio alianza kuirekodi kabla yangu mimi, vilevile Audio nyingine ambayo inarekodiwa sasa hivi ni ya TYGA ya Young Money ndio kolabo ambayo nina hamu nayo sana, ilikua irekodiwe mwezi huu wa february lakini imesogezwa mbele na sasa itafanyika kabla ya june mwaka huu, nikitulia naweza kuianza may na kila kitu kiko kwenye mstari”

MWANAMKE AKIRI KUPATA UJAUZITO KUTOKA KWA MAITI!


Mama mmoja huko Marekani anayefanya kazi mochuari ameingia matatani baada ya kupata ujauzito kwa kujamiiana na mtu aliyekufa ambapo Mtandao wa habari wa Dead Serious News umesema tukio hilo linadhaniwa kutokea katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Mourning Glory, nje ya Lexington, Missouri.
Polisi wamemshtaki mama huyo aitwaye Felicity Marmaduke kwa kosa la kunajisi na kuchezea maiti ambapo Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na polisi, kiungo cha kiume cha mwili wa mtu aliyefariki kilihamasika wakati mwili ukioshwa.
Taarifa zinasema kwa kuwa mama huyo alikuwa peke yake, aliamua kujamiiana na mwili huo na Kwa mshangao hata kwa mwanamama huyo, maiti huyo alitoa mbegu za kiume. Wiki chache baadaye Bi Marmaduke alijikuta na ujazito.

Mkuu wa Mkoa Wa Ruvuma Said Mwambungu Aongoza Kikao Cha Kamati Ya Ulinzi na Usalama Ruvuma Kujadili Mauaji Yaliyoikumba Mkoa Wa Songea

Baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo, wakiwa katika mkutano wa kujadili mtafaruku huo. Add caption
 Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi ya Mkoa wa Ruvuma, ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo, Said Mwambungu akizungumza katika mkutano na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama baada ya kutokea mauaji wakati wa maandamano ya wananchi ya kupinga mauaji ya watu kwa imani za kishirikina.. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea, Thomas Sabaya.

Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambao ni wenyeviti wa Serikali za mitaa, madiwani wakimsikiza Mwambungu kwenye mkutano huo wa dharula.Picha na Muhidin Amri

SOMALIA BADO KWA MOTO, SOMA ILICHOSEMA UN WAKATI HUU

Majeshi ya Ethiopia na yale ya serikali ya mpito ya Somalia yameuteka mji wa Baidoa ambao ni mojawapo ya ngome kuu ya wapiganaji wa Al Shabaab ambapo Walioshuhudia wamesema magari 50 vikiwemo vifaru vya kivita viliingia mjini Baidoa bila upinzani wowote.
Kundi la Al-Shabaab ambalo lilijiunga rasmi ya mtandao wa al-Qaeda limethibitisha kuwaondoa wapiganaji wake kutoka mji huo ambapo pia Wapiganaji hao wameonya kuanzisha mashambulio ya kujitoa mhanga dhidi ya majeshi ya kigeni.

Rais Jakaya Kikwete Ashuhudia Utiwaji Saini MOU Ya Kupeleka Washtakiwa Wa Uharamia Wa Kisomali Katika Jela Husika


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri masuala ya Jumuiya ya Madola, Umoja wa Mataifa  na Afrika na Mazingira(Parliamentary Under Secretary responsible for Africa, United Nations, economic issues,conflict resolution,and climate change)  wa Uingereza Bw  Hendry Bellingham wakishuhudia Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa  Mh Bernad Membe akiweka saini sambamba na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza kuhusu makubaliano kati ya nchi hizo mbili juu ya taratibu za  kukabadhiana watuhumiwa wa uharamia na mali zilizokamatwa katika matukio ya uharamia katika bahari kuu leo February 23, 2012 Lancaster House,London.Picha na IKULU

Wednesday, 22 February 2012


WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA MUUNGANO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO ZANZIBAR

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan akionyeshwa kito kinachotengeneza Lulu ambayo hufanywa Pete na Katibu wa Kampuni ya Ukweli ni Njia Safi Bi Safia Hashim alipotembelea kikundi cha akina mama cha Bweleo Wilaya ya Magharibi Unguja wakati wa Ziara yake ya kuangalia Miradi ya Maendeleo ya [TASAF] inafadhiliwa na Serikali ya Muungano.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Muugano Samia Suluhu Hassan akipata Maelezo kwa Bi Mwajuma Mwinyi kuhusu Matumizi ya Mwani wa Baharini ambao wanatengenezea Sabuni ya Kuogea na huweka Unyevunyevu kwenye ngozi kuifanya nyororo wakati wa Ziara yake ya kutembelea Miradi ya Maendeleo inayofadhiliwa na Serikali ya Muugano huko Bweleo Wilaya ya Magharibi Mjini Unguja[Picha na Ali Meja]


======== =====    =====================  ==============
 Na Ali Issa Maelezo.

Mamlaka ya kusimamia uvuvi wa bahari kuu Tanzania imeimba serikali ya jamuhuri ya muungano Tanzania na ile ya Zanzibar  kuiridhia  sheria ilopo na kuipitisha  iliweze kufanya kazi zake vizuri na kutekeleza vyema kazi zake  mamla.

Hayo yamesemwa leo huko kinazini katika jengo la ZSTC Zanzibar  na   Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Geofrey Frank Nanyaro  wakati wamazungumzo kati ya malaka na Ofisi inayo shughulikia masuala ya muungano Tanzania mbele ya waziri  Samia Suluhu Hasani aliofika hapo akiwa ziarani kutembelea maeneo hayo .

Amesema malaka ya kusimamia bahari kuu ni taasisi ilio undwa kupitia sheria ya malaka ya kusimamia uvuvi kwenye eneo la ukanda wa kiuchumi EEZ ya mwaka 1998 ambayo ilifanyiwa marekebisho kupitia sheria namba nne ya mwaka 2009 sheria  ambayo ilishirikishA Pande zote mbili za muungano  na badalayake ikapelekwa baraza la mawaziri na  kukubaliwa lakini upande wa pili wa  baraza la wawakilishi hadisasa bado kuridhia sheria hiyo .

Amesema kuchelewa kuridhia sheria hiyo nikufanya kazi katika mazingira ambayo hayaendani  na kazi kisheria na  kuyafanya kuwa mazingira  magumu katika utekelezaji wakazi zake kitalamu  .

“Nivigumu kutekeleza kazizetu kitaalamu kwani sheria ndio inayo muongoza mtu kufanyakazi vyema hivyo  ikawa sheria haijaridhiwa itakuwaje juu yakusimamia baharikuu ambao wanao kuja kuvua wanafahamu kilakitu .”alisema Geofrey .  Aidha mkurugenzi huyo alisema kuwa kuchelewa kuridhiwa kwasheria hiyo kuna wakosesha frusa wataalamu wao hata kupata  mafao yao kimsingi  kamavile mishahara nahatimae kupata posho tu.  Amesema halihiyo haipendezi kwani inaleta uchovu katka uwajibikaji na misingi boa ya kazi .

Nae mtaalamu wamtambo unao toa ripoti za meli za kigeni zinazo ingia nchini Damian Boniface Chando amesema kua Malaka hiyo hivisasa inauwezo wa kugundua meli zinazo ingia  na kutoka kaita ukanda wa baharikuu  zinazo vuasamaki  kinyemela kwa kutumia mtambo wa Vessl monitoring system ambao wanao na  unafanyakazi muda wote.

Aidha alisema kuwa mtambo huo unaweza usifanye kazi iwapo mabaharia watafanya uharamia kwa kuzima kifaa   kiitwacho kwa kitaalamu transimitter na wao wasiweze kundua kama samaki wao wanavuliwa kwa kuibiwa. “Ni vizuri kujipanga kua na doria kwani mtambo huu hautoshi pekeyake iwapo mabaharia watafanya uharamia bila  ya  kuomba kibali na kuzima mitamboyao’alisema Boniface  . 

Nae waziri samia alisema wanazichukuwa changamoto zilopo na kwenda kuzifanyiakazi, lakini alisema kua  wakati umefika kwa viongozi kuwa wa wazi na wakweli wanapokuwa katika vikao  na kutekeleza yale wanayo yasema,Amesema katika ziara yake amejifunza    mengi ambayo alikuwa hayajui na sasa anaelewa na atayapeleka munamo husika na kufanyiwa kazi.

Wazirihuyo alitembelea mamlaka ya Uvuvi wa Bahari kuu Fumba Maradi wa MACEP Bweleo  kuangalia madawati yalio na TASAF skuli ya kombeni pamoja na mradi wa kinamama wakutengeneza sabuniza kuogea kwamalighafi ya mwani napete za luu kwamalighafi ya kombe za baharini. 

BENKI YA NBC YAJITOSA KUDHAMINI GOFU LA WANAWAKE NCHINI

Meneja Udhamini na Matukio wa NBC, Bi. Rachel Remona Kimambo (wa pili kushoto) akikabidhi mfani wa hundi ya shs milioni kwa Nahodha wa Kitengo cha Gofu ya Wanawake cha Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam,Vivienne Mwaulambo kusaidia mashindano yao yanayotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo katika klabu hiyo jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni maofisa wa NBC na viongozi wa kitengo hicho cha gofu.
Nahodha wa Kitengo cha Gofu ya Wanawake cha Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam, Vivienne Mwaulambo (kushoto) akizungumza kabla ya kupokea msaada msaada huo kutoka benki ya NBC. Katikati ni Meneja Udhamini na Matukio wa NBC, Bi. Rachel Remona Kimambo na kulia ni Katibu wa kitengo, Joyce Svarva.
Maofisa wa NBC pamoja na wa Kitengo cha Gofu ya Wanawake cha Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam wakipiga picha ya pamoja katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Nahodha wa Kitengo cha Gofu ya Wanawake cha Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam, Vivienne Mwaulambo (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya maofisa wa NBC baada ya kupokea msaada msaada huo kutoka benki ya NBC.Kutoka kushoto ni, Arden Kitomari, Meneja Chapa na Matangazo, Eddie Mhina; Mshauri wa Mawasiliano na Meneja Udhamini na Matukio wa NBC,Bi. Rachel Remona Kimambo.

DK. NAGU AKUTANA NA UJUMBE WA WAWAKILISHI WA UCHUMI NA BIASHARA KUTOKA CHINA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dk. Mary Nagu akiongea jambo na aliyekuwa Mwakilishi Mkuu wa Uchumi na Biashara wa watu wa Jamhuri ya China nchini Tanzania Zhao Zhongqiu leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam . Zhongqiu alimtembelea waziri huyo kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dk. Mary Nagu akisalimiana na Mwakilishi Mkuu mpya wa Uchumi na Biashara wa watu wa Jamhuri ya China nchini Tanzania Lin Zhiyong leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam . Zhiyong anachukua nafasi ya Zhao Zhongqiu ambaye amemaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dk.Mary Nagu akiongea na ujumbe wa wawakilishi wa Uchumi na Biashara wa watu wa Jamhuri ya China nchini Tanzania walipomtembelea leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam . Ujumbe huo uliongelea mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na jinsi ya kuimarisha mahusiano ya kiuchumi na kibiashara kati ya Tanzania na China.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dk.Mary Nagu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Uchumi na Biashara wa watu wa Jamhuri ya China nchini Tanzania walipomtembelea leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Lin Zhiyong ambaye ni Mwalikishi mpya na kulia ni Zhao Zhongqiu ambaye amemaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini.Picha na Anna Nkinda - Maelezo.