Wiki mbili baada ya washiriki wa tuzo za KTMA mwaka huu kutangazwa huku Diamond Platnums akiwa amechaguliwa kwenye category nyingi zaidi, msanii huyo amekiri kwamba mpaka sasa ni lazima akubaliwa kwamba Tuzo 3 za KTMA mwaka juzi zimeleta mabadiliko makubwa sana kwenye maisha yake.
Amesema “kwanza zilininyanyua na kujulikana kwenye nchi mbalimbali Afrika na hata nilipokua najitambulisha nilikua najitetea kwa ushahidi wa tuzo hizo”
Naseeb amekubali kwamba kupata tuzo hizo kulimfanya apandishe hata bei ya kupiga showz, “nakumbuka kipindi hiko kwa sababu ndio nilikua naanza nilikua na wimbo mmoja wa kamwambie japokua nilikua nimetoa video ya single ya Mbagala na nilikua nafanya show kwa laki tano mpaka laki sita lakini kwa sasa bei zimebadilika”
Show za Bongo Diamond anaanza kupiga kuanzia milioni 2, na za nje ya nchi ni kuanzia dola za kimarekani elfu 3mpakaelfu 5. 
No comments:
Post a Comment