Friday, 19 October 2012

TAARIFA KAMILI KUHUSU VURUGU ZA ZNZ SASA HIVI NA ASKARI ALIYEUWAWA.



Mpaka sasa hivi hali katika baadhi ya vitongoji visiwani Zanzibar sio shwari pamoja na kwamba serikali imetoa tamko kuwataka wananchi kuendelea na shughuli zao kama kawaida.
Vurugu zilianza toka jana kutokana na kukamatwa kwa kiongozi wa taasisi ya kiislamu, Sheikh Farid Hadi Ahmed ambapo msemaji wa polisi Znz Mohamed Mhina amesema mpaka leo wafuasi wa kikundi cha Uamsho wameendelea na vurugu na uchomaji wa matairi barabarani na kuweka mawe.
Kwenye sentensi nyingine ni kwamba leo ndio imethibitishwa kuuwawa kwa  askari polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia FFU Saidi Abdul-Rahman, ameuwawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.
Pamoja na watu waliofanya tukio hilo kutofahamika msemaji wa polisi Mhina amesema wanaosadikiwa kufanya hilo tukio ni wafuasi wa kikundi cha Uamsho ambapo mwili wake imepatikana na imefanyiwa uchunguzi kwenye hospitali kuu ya mnazi mmoja.
Mpaka sasa watu 10 wamekamatwa kutokana na fujo hizo vilevile Polisi wanaendelea kutafuta mahali alipo kiongozi wa kikundi cha Uamsho ambae alidaiwa kupotea tangu juzi jioni (jumanne) ambapo alimtuma dereva wake apeleke umeme nyumbani, dereva aliporudi kumfata hakumkuta.

Unaweza kumsikiliza Wakili wa Sheikh Ponda hapo chini…

TAARIFA KAMILI KUHUSU WAUMINI 50 WA DINI YA KIISLAMU KUFIKISHWA MAHAKAMANI LEO DSM.



Jumla ya waumini 50 wa Dini ya Kiislamu, ambao ni wafuasi wa Sheikh ISSA PONDA pamoja na yeye mwenyewe, leo wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, kujibu kesi ya wizi wa mali na uvamizi wa Ardhi inayowakabili.
Washitakiwa hao 50 kwa pamoja wanakabiliwa na Mashitaka Manne, yakiwemo ya kula njama kwa nia ya kutenda kosa kinyume cha sheria, kuingia kwa nguvu kwa lengo la kutaka kutenda makosa, kumiliki kwa nguvu ardhi ya Kampuni ya AGRI-TANZA, wizi wa matofali 1,500, na kokoto tani 36 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 56.6.
Wakili mwandamizi wa Serikali TUMAINI KWEKA, amesema kuwa pamoja na makosa hayo manne, mtuhumiwa namba moja Sheikh ISSA PONDA anakabiliwa na shitaka jingine la Tano, la uchochezi wenye nia ya kutaka kutenda kosa.
Akisoma mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi STEWART SANGA, wa Mahakama ya Haklimu mkazi Kisutu, aliyemuwakilisha Hakimu Mkazi Mfawidhi VICTORIA NONGWA ambaye yupo kwenye Semina, Wakili KWEKA ameitaka mahakama itoe masharti magumu kwa washitakiwa 49, ili watakapotoka wasirejee kwenda kutenda makosa.
Kwa upande wa mshitakiwa wa kwanza Sheikh PONDA, Wakili KWEKA amesema kwamba Mwendesha mashtaka Mkuu wa Serikali DPP ELIEZA FERESHI, ameiandikia mahakama kuitaka kutompatia dhamana mshitakiwa huyo, kutokana na sababu za Kiusalama na Maslahi ya Jamuhuri, jambo ambalo limepingwa na wakili wa washitakiwa JUMA NASSORO, aliyetaka kuainishwa kwa sababu zaidi za kutotaka dhamana hiyo.
Licha ya kupinga agizo hilo la DPP pia Wakili NASSORO ameiomba mahakama, kumlegezea masharti mshitakiwa mwenye umri mkubwa kuliko washitakiwa wote, aliyemtaja kwa jina la ZAIDA YUSUPH mwenye umri wa miaka 100, kutokana na hali yake ya kiafya.
Kabla ya uamuzi wa Hakimu, Wakili KWEKA ameiambia mahakama kuwa haina uwezo kisheria wa kupinga maagizo yaliyotolewa na DPP, hivyo ombi la wakili wa washitakiwa haliwezi kufanyiwa kazi.
Baada ya maelezo ya mawakili hao, Hakimu STEWART SANGA amesema hawezi kusikiliza ombi lolote wala kutoa maamuzi, kutokana na kutokuwepo kwa hakimu mwenye dhamana ya kusikiliza kesi hiyo, na hivyo kuwataka watuhumiwa wote kurudi Rumande mpaka Novemba Mosi, ambapo kesi hiyo itatajwa tena.
Sheikh PONDA aliwasili katika viwanja vya mahakama ya Kisutu majira ya Saa sita na dakika ishirini, akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi, ambapo kesi ilianza kusomwa na kudumu kwa zaidi ya saa moja, huku ndugu wa washitakiwa wakiwepo nje kusubiri hatma ya ndugu zao.

Wednesday, 3 October 2012

BREAKING NUUUUUUUUZ: AJALI MBAYA IMETOKEA MBALIZI MBEYA MAGARI MAWILI YAMEGONGANA NA KUWAKA MOTO... WATU KUMI WAMEFARIKI DUNIA HAPO HAPO.


Breaking nuuuuuuuuz: Ajali mbaya imetokea mbalizi Mbeya magari mawili yamegongana na kuwaka moto... watu Kumi wamefariki dunia Hapo hapo. Tukio kamili linakuja Punde .. Fuatilia www.mbeyayetu.blogspot.com

MELI MPYA YA KISASA YA AZAM MARINE YENYE UWEZO WA KUBEBA ZAIDI YA WATU 1000 NA MAGARI 200 YAWASILI NCHINI.

 Baadhi ya wakazi wa Zanzibar wakipiga picha Meli hiyo iliyowasili Visiwani Zanzibar leo.
 Meli ya Azam Marine inayoitwa Azam SeaLink 1 ikiwasili katika bandari ya Visawani Zanzibar kwa mara kwanza.
 Mzee Said Bakheresa (mwenye nguo nyeusi) akikagua mazingira ya Meli hiyo baada ya kuwasili Bandari ya Zanzibar leo.
 Sehemu ya Parking yenye uwezo wa kuingiza magari 200.

Muonekano wa ndani wa Lounge ya kumpzikia wasafiri.

Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar

Kampuni ya Azam Marine inayomiliki boti ziendazo kasi hapa nchini, leo imeingiza meli mpya na ya kisasa itakayochukua zaiidi ya abiria 1500 na magari 200.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Azam Marine, Bw. Hussein Mohammed Saidi, amesema leo mjini Zanzibar kuwa meli hiyo ambayo itafanya safari zake kati ya Dar es Salaam, zanzibar na Pemba itatoza nauli nafuu kwa abiria wake.

Amesema meli hiyo ambayo inatarajiwa kuanza safari zake mara baada ya kukamilisha taratibu za mamlaka mbalimbali.

Meli hiyo inayoitwa AZAM SEALINKI ni ya kisasa katika ukanda huu wa Mwambao wa nchi za Kusini na Pembe ya Afrika.

Bw. Hussein amesema Meli hiyo ambayo imetengenezwa nchini Ugiriki na inatayarishiwa eneo maalumu litakalotumika kwa kupakia na kushusha abiria na mizigo yakiwemo magari.

Amesema meli hiyo itasafiri kwa muda wa saa tatu kutoka Dar es salaam na Zanzibar na saa 4 kutoka Zanzibar na Pemba ama saa 7 kutoka dar es salaam na Pemba.

Amesema pamoja na kuwasili kwa Meli hiyo, Kampuni ya Azam pia inatarajia kuleta meli nyingine ya abiiria inayojulikana kama Kilimanjaro namba 4.

Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wa Visiwa vya zanzibar wamepongeza ujio wa meli hiyo lakini wakaitaka serikali kuendelea kudhibiti uingizwaji wa meli chakavu na kukuu ili kuepuka uwezekano wa kutokea ajali za mara kwa mara.

Bwana Rajabu Khamisi mkazi wa Pemba na Bi. Rehema Omari wa mjini Zanzibar, wamesema kuna haja ya Serikali kusimamia ukomo wa nauli ili kila mwananchi aweze kusafiri kutoka sehemu moja na nyingine kwani wamesema vipato havilingani.

RICK ROSS WA BONGO KUMPOKEA AIRPORT RICK ROSS WA MAREKAN

                                       Rick Ross Kutoka USA
Rick Ross Ajipange atapokuja Tanzania Tarehe 06 Oct 2012 kukutana na look i like wake....huendi Baba ake alicha mbegu Bongo..lol.
 Rick Ross wa Bongo kumpokea airport Rick Ross wa Marekani, ama kweli duniani wa wili wa wili
Rick Ross wa Bongo huyu hapa

Jinsi Basi la Dar Express Lilivyowaka Moto Njia Panda ya Dar,Arusha,Tanga(Segera)


Basi la  Dar Express limepata ajali ya kuungua moto leo asubuhi katika njia panda ya Dar, Arusha, Tanga (Segera) hakuna mtu aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha. Katika ajali hiyo mizigo yote iliteketea kwa moto huo ambapo abiria wengi waliokuwamo kwenye gari hilo walikuwa ni wanafuzi.Picha na Samweli Mikuza