Monday, 1 July 2013

TUJIKUMBUSHE MAMBO MACHACHE YANAYOTENDEKA KUHUSU OBAMA AMBAYE TAYARI YUPO TANZANIA

Obama akiwa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete Rais wa Marekani Barack Obama amewasili nchini Tanzania leo Jumatatu kwa zara ya siku mbili, ikiwa ni kituo chake cha mwisho cha ziara yake barani Afrika akitokea nchini Afrika Kusini. Obama ambaye ameambatana na mkewe Michelle Obama amepokelewa na mwenyeji wake rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Salma Kikwete katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na kisha kuelekea Ikulu ya rais. Rais wa Marekani akicheza muziki wa band wakati alipotua uwanjani    Rais Obama na mwenyeji wake wanatarajiwa kufanya mazungumzo ya pamoja ikulu.

No comments:

Post a Comment